Wednesday, 24 September 2014

Wizara ya Mambo ya Nje ya Misri imetangaza kuwa Wapalestina na Israel wamekubaliana kuendeleza mazungumzo kuhusiana na makubaliano ya usitishaji vita. Mahmoud al Zahar mmoja wa viongozi wa harakati ya Hamas ya Palestina pia ameeleza kuwa ujumbe wa Palestina umeamua kuendeleza vikao vya Cairo baada ya kushauriana na wanachama wa harakati hiyo ndani na nje ya Ghaza. 
Kabla ya hapo, baadhi ya duru za habari za Palestina ziliripoti kuwa, ujumbe wa Palestina unachunguza kujiengua kwenye mazungumzo ya Cairo ikiwa ni jibu na radiamali kwa kuuliwa wanachama wawili wa muqawama huko al Khalil. Wazayuni ambao wanadai kuwa  Amar Abu Aisha na Marwan  al Qawasmih wanachama wa brigedi za Izzuddin al Qassam tawi la kijeshi la Hamas walihusika kuwateka nyara na kuwauwa walowezi watatu wa Kizayuni huko al Khalil, jana asubuhi waliwaua shahidi wanaharakati hao.


0 comments:

Post a Comment

Translate

facebook

TANGAZA HAPA

KWA HABARI MAKINI

Napokea maoni muhimu kwa pale unapoona apakustahili kuwepo kwenye blogg yetu makini yenye lengo la kukuunganisha pamoja na kuelimishana kwa yale mazuri yote piga simu kwa chochote muhimu namba zipo apo juu

NEWS