Viongozi wa dunia wameahidi dola bilioni 2.3 katika mkutano wa
Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi, kwa lengo la kusaidia
maendeleo ya nchi katika kukabiliana na madhara yanayotokana na ongezeko
la joto la dunia. Mwishoni mwa kikao hicho Katibu Mkuu wa Umoja wa
Mataifa Ban Ki Moon ametoa wito wa kufanywa jitihada za kufikiwa
makubaliano ya dunia ya tabianchi ifikapo mwaka kesho, na kuwataka
viongozi wa dunia watekeleze majukumu yao katika kulinda sayari ya dunia
kwa kupunguza joto la dunia kwa nyuzi joto 2.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa pia ametaka viongozi wa dunia wachukue hatua zaidi za kupunguza gesi za nyumba ya kioo, kuzuia kukatwa misitu na kusaidia nchi masikini kukabiliana na madhara ya mabadiliko ya hali ya hewa kama vile ukame, mafuriko, vimbunga na kupanda kiwango cha maji ya bahari.
Kwa muda mrefu sasa nchi zinazoendelea zimekuwa zikitaka kusaiiniwe makubaliano kuhusu tabianchi bila kujali ahadi za Marekani, zikisema kuwa nchi hiyo tajiri na iliyoendelea ndiyo inayochangia pakubwa katika kuharibu hali ya hewa duniani.

0 comments:
Post a Comment