Tuesday, 1 July 2014

Jirani wa rais Robert Mugabe wa Zimbabwe amepigwa faini kwa kuachia mbwa wake kuwinda katika eneo la rais huyo, limeripoti gazeti la serikali.
Mahakama ilimhukumu jirani huyo, Michael Pazarangu kulipa dola 50 au kwenda jela kwa siku 30, limesema gazeti la Herald.

Ametuhumiwa kwa kuwaachilia "mbwa wake wakali kuranda randa huru" katika nyumba binafsi ya rais mjini Harare. Mahakama iliambiwa kuwa mbwa wa bwana Pazarangu waliua swala ndani ya eneo la Rais Mugabe mwaka jana. Mbwa hao inadhaniwa waliingia katika eneo la Mugabe kupitia tundu kwenye uzio unaotenganisha nyumba hizo mbili katika eneo la Borrowdale.
 Beba mgongoni usimwachie akizulula utakwenda jela hata wewe mfugaji mbwa olela jifunze hapa

0 comments:

Post a Comment

Translate

facebook

TANGAZA HAPA

KWA HABARI MAKINI

Napokea maoni muhimu kwa pale unapoona apakustahili kuwepo kwenye blogg yetu makini yenye lengo la kukuunganisha pamoja na kuelimishana kwa yale mazuri yote piga simu kwa chochote muhimu namba zipo apo juu

NEWS