Tuesday, 1 July 2014

"SABABU ZA MTATIRO KUNG’OKA CUF" - Hii nimeinasa Tanzania Daima…………Inasema;

SIRI ya Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahimu Lipumba kufanya mabadiliko kwenye kurugenzi zake kwa kumng’oa Julius Mtatiro kwenye nafasi ya Naibu Katibu Mkuu Bara, imefichuka.

Vyanzo vya habari kutoka ndani ya chama hicho, vinadai kuwa sababu ya kwanza imetokana na viongozi wakuu wa chama hicho taifa kumtaka Mtatiro asigombee nafasi yoyote.

Inaelezwa kwamba Mtatiro aliandaliwa kisaikolojia kwamba hatarudi kwenye nafasi yake kwa madai ya kutoridhishwa na utendaji wake.

Sababu ya pili ambayo inatajwa na baadhi ya viongozi wa CUF ni kwamba kiongozi huyo kijana, anadaiwa kujihusisha na matumizi mabaya ya fedha hasa wakati wa kampeni za uchaguzi mdogo wa Igunga.

Kwa mujibu wa habari hizo, sababu ya tatu inaelezwa kuwa Mtatiro alikuwa akifanya siasa za kitoto (siasa nyepesi), zilizokuwa zinawakera baadhi ya viongozi wa juu wa CUF.

“Mtatiro sio kama amependa mwenyewe kuacha nafasi hiyo la hasha, ukweli ni kwamba aliandaliwa kisaikolojia kuwa nafasi hiyo hatoshi na inamlazimu atoke ampishe Sakaya ambaye anaweza akasukuma gurudumu hilo la chama,” kilieleza chanzo cha habari hizo.
______________________________________________________

Hii habari imenishangaza sana….Tanzania Daima nalo limegeuka kuwa gazeti la kuandika habari za kubahatisha namna hii…kwani hamna vyanzo vya habari sahihi???? nilitegemea UHURU ndo wahangaike kuandika habari zisizo na kichwa wala miguu ….tusubiri tena kesho watakuja sijui na sababu zipi. KUPUMZIKA KWANGU WADHIFA WA JUU NDANI YA CUF KUMEGEUZWA KUWA DEAL…..Nigawieni basi MGAO wangu mkishauza magazeti kwa habari za Uzushi!!!!!

0 comments:

Post a Comment

Translate

facebook

TANGAZA HAPA

KWA HABARI MAKINI

Napokea maoni muhimu kwa pale unapoona apakustahili kuwepo kwenye blogg yetu makini yenye lengo la kukuunganisha pamoja na kuelimishana kwa yale mazuri yote piga simu kwa chochote muhimu namba zipo apo juu

NEWS