Idadi ya wakimbizi wa Burundi waliokimbilia nchi jirani kufuatia ghasia
zinazoendelea nchini mwao imeongezeka na kufikia elfu ha
msini katika wiki moja iliyopita pekee
Idadi ya wakimbizi wa Burundi waliokimbilia nchi jirani kufuatia ghasia zinazoendelea nchini mwao imeongezeka na kufikia elfu hamsini katika wiki moja iliyopita pekee. Hiyo ni kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) ambalo limesema raia hao wamekimbilia Rwanda, Tanzania na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Idadi kubwa ya wakimbizi wamekimbilia Rwanda na sasa Tanzania baada ya vizuizi vya kuingia kuondolewa na wengi wao ni wanawake na watoto wakikumbwa na madhila. Adrian Edwards, msemaji wa UNHCR, Geneva amesema kuwawanawake wengi wameripoti kubakwa na watu wenye silaha, mbali na madhila mengine, wakihonga ili waweze kupita kwenye vizuizi barabarani huku wengine wakitembea saa nyingi porini wakiwa na watoto wao. UNHCR imetoa wito kwa mamlaka za Burundi kuruhusu watu watembee kwa uhuru, na muhimu mipaka ikabakia wazi.
Katika kipindi cha wiki mbili zilizopita Burundi imekumbwa na machafuko na ghasia kufuatia tangazo la Rais Pierre Nkurunziza kuwa atawania urais kwa muhula wa tatu. Takribani watu 15 wamepoteza maisha katika ghasia hizo. Wapinzani wanasema Nkurunziza anakiuka Mapatano ya Arusha yaliyomaliza vita vya ndani nchini humo, lakini wafuasi wa rais huyo wanasema katika muhula wake wa kwanza Nkurunziza alichaguliwa na Bunge na hivyo muhula huo hauwezi kuhesabiwa.
jiunge nasi kwa ku LIKE page yetu ya facebook/millanzy.blogspot.com

0 comments:
Post a Comment