Sunday, 8 March 2015

Afisa wa ngazi ya juu wa Ujerumani ametaka kuangaliwa upya sera za Ujerumani za kuiuzia silaha Saudi Arabia akiitaja nchi hiyo ya kifalme kuwa inaongoza kwa kutuma magaidi katika eneo la Mashariki ya Kati. Claudia Roth Makamu Mwenyekiti wa bunge la Ujerumani (Bundestag) amewasilisha ombi hilo wakati alipofanya mahojiano na gazeti la Ujerumani la Welt am Sonntag. Makamu Mwenyekiti wa bunge la Ujerumani ameitaja Riyadh kuwa ni mtumaji mkuu wua magaidi Mashariki ya Kati na kuongeza kuwa, idadi kubwa ya wanamgambo wenye misimamo mikali walioko Syria, Afghanistan na Iraq wametoka Saudi Arabia. Claudia Roth mwanasiasa wa chama cha Kijani cha nchini Ujerumani ametaka pia kuachiwa huru mwanaharakati Msaudia Raif Badawi ambaye amehukumiwa kifungo cha miaka kumi jela na viboko 1000. Saudi Arabia ni moja ya nchi wanunuzi wakuu wa silaha za Ujerumani.



0 comments:

Post a Comment

Translate

facebook

TANGAZA HAPA

KWA HABARI MAKINI

Napokea maoni muhimu kwa pale unapoona apakustahili kuwepo kwenye blogg yetu makini yenye lengo la kukuunganisha pamoja na kuelimishana kwa yale mazuri yote piga simu kwa chochote muhimu namba zipo apo juu

NEWS