Wednesday, 9 July 2014

Madee alipigiwa simu na jamaa mmoja kisha kujitambulisha kuwa ye ni Jabirr Salehe mtangazi wa Times Fm anashida na ela kidogo kwani mke wake anahitaji kufanyiwa opalesheni kwenye hospital ya taifa ya Muhimbili
Madee alijua dhahili kuwa uyu anaeongea sio Jabirr kwani hata yeye kuna staili ambayo uwa wanaitana 
akaona isiwe tabu akamjibu kuwa kwa sasa naendesha gari nikishuka nitakupigia 
baada ya kupita dakika kadhaa Madee akamlukia ewani mshikaji na kumsikiliza jamaa akafunguka zaidi na kusema anaomba ikiwezekana atumiwe sasa ivi kwenye namba iyo aliyompigia nayo
ndipo Madee akamjibu habari za Tigo pesa mimi sina nazo we kama vipi ibuka Manzese ela ipo,
jamaa akasema poa, jamaa akamtuma muendesha bodaboda akawa anawasiliana na Madee adi Manzese Tip Top kisha jamaa alipofika cha kwanza Madee akachukua funguo ya piki piki
na kumuuliza wewe uyo Jabirr unamjua jamaa aliyetumwa akapiga kimya akasema mi nimetumwa nije kuchukua ela hapa
Madee akampokonya simu ili asipoteze muda na kisha kwenda na kitaa ambako walikuwepo madee na akina babu Tale , yule jamaa ilibidi tu wamchukulie simu zake na 2 kisha madee akamtumia sms (ujumbe wa maandishi) kuwa teali jamaa nimeshampa mzigo
kumbuka wakati uo ile simu ya mwendesha boda boda ipo mikononi mwa Madee baada ya kutuma ile sms jamaa akawa anampigia mwendesha boda baadae Madee 
  jamaa alivyoona kwa Madee kimebuma akampigia simu Shetta na kumwambia vile vile na namba ile ile
na kusisitiza anaomba namba ya Diamond Platnumz, majibu ya Shetta nikuwa ebwane sina ela kwa sasa
nikiwa nayo nitakutumia, ndani ya dakika chache Shetta akaenda kwa babu Tale Magomeni si ndipo wakakutana na akina Madee wakiwa kwenye stori ya kupigiwa simu nae Shetta akasema nami nimepigiwa simu kama iyo na namba iyo iyo, pale jamaa katika mtego ule alikuja kudakwa na 
akina Mkubwa Fella lakini aliwatoka akiwa nako kapokonywa simu zake mbili na viwalo kadhaa kavuliwa iyo ndio habari ya utapeli Bongo DSM akuishia apo
wapekua simu ya jamaa na kukuta kawatumia ujumbe wa maandishi wasanii wengi sana akiwa taka wampe pesa kwa ajili ya matibabu ya mkewe
Madee atoa wito kwa wasanii wenzake na kusema hata kama auna namba za mtu usika anaetumiwa kwenye jina lake kwa kuhitaji kitu flani jaribu kwa watu wake wa karibu kupata uhakika zaidi
 PICHANI NDIYE MTANGAZAJI ALISI ANAYETUMIWA JINA LAKE KWENYE UTAPELI
ANAITWA Jabirr Salehe A.k.a kibonge Tozi 

Jabirr nae amesikitishwa na utapeli uu kwani sio vizuri na kusema 
moja ya vitu ambayo kwanza hana ni MKE
kwaiyo kwa wanano mjua kibonge tozi lazima washangae kuwa jamaa ameoa lini
na kumtaka mtu yoyote mwenye wazo au tabia ya kutumia jina la mtu kwa utapeli ataishia pabaya


0 comments:

Post a Comment

Translate

facebook

TANGAZA HAPA

KWA HABARI MAKINI

Napokea maoni muhimu kwa pale unapoona apakustahili kuwepo kwenye blogg yetu makini yenye lengo la kukuunganisha pamoja na kuelimishana kwa yale mazuri yote piga simu kwa chochote muhimu namba zipo apo juu

NEWS