Sunday, 6 July 2014

  Mabalozi wamekuwa wakitumika sana na chama cha cha mapinduzi kwa kuwatumia katika kutisha wananchi wanao kuwa wanachama wa vyama vya upinzani hasa CHADEMA kwa kuwasingizia kesi, pia hutumiwa kama ni viongozi wa kiserikali kitu ambacho kisheria mabalozi siku zote ni viongozi wa vyama kwa shughuli za vyama na si kwa shughuli za kiserikali, lakini imekiwa ni tatizo kubwa sana kwani vijijini wananchi
  hawana uelewa kabisa wanawasujudia mabalozi km viongozi ambao waliwachagua wakati sio kweli, sheria ya serikali za mitaa kwa ngazi ya kijiji inatambua uwepo wa nafasi ya mwenyekiti kitongoji/mtaa,mwenyekiti kijiji na wajumbe wa serikali na hizo nafasi zote zinagombaniwa na watu kuchaguliwa na mikutano mikuu ya uchaguzi serikali za mitaa, wakati mabalozi
  wanapatika kwa kuchaguliwa na wanachama wa vyama vyao, sasa kama kichwa cha habari changu ni research niliyofanya kwa takribani 80% ni kikwazo kwa ustawi wa demokrasi, kwani wamekuwa wachungaji/mashehe kusuruhisha ndoa za wananchi lakini pia wamekua majaji na màhakimu kwa kuhukumu kesi pindi inapotokea wananchi wawili kutofauti, wenyeviti wa vitongoji/mitaa
wameshindwa kuwajibika sababu mfumo Huu umekuwa wa kawada kwa sababu unakinufaisha chama tawala CCM,, nikiwa kama kiongozi wa jimbo la Ismani ndilo tatizo kubwa kwa nchi nzima!

0 comments:

Post a Comment

Translate

facebook

TANGAZA HAPA

KWA HABARI MAKINI

Napokea maoni muhimu kwa pale unapoona apakustahili kuwepo kwenye blogg yetu makini yenye lengo la kukuunganisha pamoja na kuelimishana kwa yale mazuri yote piga simu kwa chochote muhimu namba zipo apo juu

NEWS