Tuesday, 8 July 2014




Taarifa kutoka wilaya ya Lamu iliyoko Pwani ya Kenya, zinaeleza kwamba wananchi waliojawa na woga kutokana na mashambulizi ya mara kwa mara wamekuwa wakilala vichakani, wakihofia kuvamiwa ndani ya nyumba zao usiku. 
Jeshi la Polisi pamoja na kikosi cha Msalaba Mwekundu wakiwa katika eneo la tukio

Leo hii wakazi wa eneo la Hindi ambako watu zaidi ya 20 waliuawa katika mashambulizi ya Jumamosi iliyopita, asubuhi ya leo wamefanya maandamano makubwa na kufunga barabara inayounganisha eneo lao na Mombasa, na kutoka mahali hapo Daniel Gakuba amezungumza na Eric Kilakya, mkuu wa kituo cha Redio cha Sifa FM na kwanza alimuuliza ni nini hasa malalamiko ya wananchi hao ? Kusikiliza mazungumzo hayo bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini.

0 comments:

Post a Comment

Translate

facebook

TANGAZA HAPA

KWA HABARI MAKINI

Napokea maoni muhimu kwa pale unapoona apakustahili kuwepo kwenye blogg yetu makini yenye lengo la kukuunganisha pamoja na kuelimishana kwa yale mazuri yote piga simu kwa chochote muhimu namba zipo apo juu

NEWS