Thursday, 26 June 2014


Chadema kwa kushirikiana na wenzetu wa Kambi rasmi ya upinzani Bungeni, tuko bize kupambana na wezi wa billioni 200 za wanyonge ambao ndio walipa kodi wa Taifa hili.

Wakati ninyi mko bize kuubomoa mfumo wa upinzani hasa Chama Kikuu cha upinzani nchini (Chadema), Sisi tumeziba sikio zetu na kuzipuuza kabisa kama sio kuzitupia kapuni propaganda zenu na tunaendeleza mapambano ya kutafuta suluhu pekee ya kuwaondolea wanyonge dhiki itokanayo na umaskini wa kupindukia kama kushinda njaa kwa mlo mmoja kwa kutwa nzima kutokana na ugumu wa maisha ya kila siku, kujifungulia sakafuni kwa kukosa vitanda mahospitalini, elimu duni n.k.

Hii ni sambamba na kupambana na mafisadi, wauzaji wa dawa za Kulevya, wanaotorosha madini yetu, Gesi yetu, mazao yetu ya misitu, wanaowadhurumu wavuvi na wakulima wa sekta zote nchini, wafanyakazi wa sekta zote, wanaosababisha tatizo sugu la ajira kwa vijana Nchini maarufu kama "Bomu linalosubiriwa kulipuka", wanaowanyanyasa machinga, mama na baba lishe wa mijini,
madereva bodaboda na daladala, wasukuma mikokoteni na troli wa mijini.

Wanaowadhurumu watoto wa mitaani haki zao za msingi za kupata elimu bora, matibabu, lishe, mavazi na malazi, wanaowadhurumu wachimbaji wadogowadogo haki zao za msingi, hususani kwenye migodi ya Dhahabu na Gesi kama vile huko Nzega Tabora, Nyamongo, Tarime Mara, Geita Gold Mine, Mwadui, Lindi, Mtwara n.k.

Hatutakaa tupoteze muda wa kujibizana na wehu wenye mizigo ya dhambi na laana ya kuwasaliti Watanzania wanaodhurumiwa kila uchao na vigogo wa Serikali hii kiziwi.

Nasema hatuwezi kupoteza muda kwa sababu tunatambua vyema kuwa wapo kazini kuwatumikia wapinga Mabadiliko na Demokrasia ili kuzinusuru familia zao dhidi ya njaa tu, lakini ipo siku mirija ya mianya ya fedha hizo chafu itakapokatwa na wahusika baada ya vibaraka hawa kushindwa kutimiza matakwa ya vigogo wanaohaha kudondoka kwenye chaguzi zijazo, wataomba kurejea kundini.

Sasa ni dhahiri kwamba, 2015 inapozidi kukaribia, ndivyo watawala wanavyozidi kupata hofu, ndivyo wanavyozidi kuwawezesha vibaraka wao ili kuudhoofisha mvumo wa mabadiliko unaohitajiwa na umma wa Watanzania mamillioni kwa mamillioni waliochoshwa na mfumo ulioshindwa kabisa kiutendaji.

Kuelekea 2015, tutashuhudia wasakatonge wanaotumiwa na watawala kupata promo ya vyombo vya habari, kulindwa na vyombo vya kiulinzi na kimaamuzi kwa lengo la kuwaondoa watanzania waliopo ndani na nje ya Nchi katika tension ya kudai mabadiliko ya mfumo huu kandamizi wa Chama legelege cha Mapinduzi.

Wanachama, Wapenzi, Wafuasi na Wakereketwa wa Chadema Nchini kote, napenda kuchukua fursa hii, kuwajulisha kuwa Chama chetu kipo imara zaidi na hakuna yeyote yule atakayeweza kukiyumbisha kwa namna yoyote ile.

Chadema tumejipanga vya kutosha kuhakikisha kwamba tunawashikisha adabu kuanzia 2015, ili wajifunze kutoka kwetu namna ambavyo viongozi wa kidemokrasia wanavyopaswa kuwa wawakilishi wa wananchi wanaofuata misingi ya utawala bora unaozingatia sheria bila shuruti, na sio kujivika udikteta wa kuwatumikisha wananchi.

0 comments:

Post a Comment

Translate

facebook

TANGAZA HAPA

KWA HABARI MAKINI

Napokea maoni muhimu kwa pale unapoona apakustahili kuwepo kwenye blogg yetu makini yenye lengo la kukuunganisha pamoja na kuelimishana kwa yale mazuri yote piga simu kwa chochote muhimu namba zipo apo juu

NEWS