Kansela wa Ujerumani Angela Markel anatazamiwa kuwasili mjini Istanbul Uturuki, hii leo kujadili kadhia ya wahajiri.
Markel anatazamiwa kukutana na kufanya mazungumzo na Rais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki kuhusu suala la wahajiri ambalo kwa sasa linaonekana kuwa zito hata kwa Umoja wa Ulaya EU.
Ziara hiyo inajiri siku moja baada ya kuripotiwa vifo vya wahajiri 12, ambao walikufa maji baada ya boti yao kuzama katika pwani ya Uturuki, ikielekea katika kisiwa cha Lesbos nchini Ugiriki.
Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia wakimbizi (UNHCR) limetangaza kuwa, wahajiri wasiopungua milioni 1.4 wanatarajiwa kuwasili barani Ulaya kufikia mwishoni mwa mwaka ujao wa 2016, na kwamba kufikia sasa wahajiri zaidi ya laki 6 wamekwisha wasili katika bara hilo.

0 comments:
Post a Comment