Wagombea 2 wa kiti cha urais kwenye uchaguzi mkuu nchini Sudan
wamejiondoa saa chache kabla ya kumalizika uchaguzi huo wakidai kuwa
tume ya uchaguzi imekiuka sheria nyingi ili kutoa mwanya kwa Rais Omar
al-Bashir kushinda kiti hicho. Ahmed Radi na Omar Awadh Al-Karim
wamesema uamuzi wao wa kujiondoa kwenye kinyang’anyiro cha urais
unatokana na kuweko ushahidi wa wazi wa ukiukwaji wa sheria za uchaguzi
na aina fulani ya udanganyifu kwa upande wa tume ya uchaguzi ya Sudan.
Tume hiyo hapo jana ilitangaza kuongeza siku moja ili kutoa fursa ya
watu zaidi kupiga kura. Uchaguzi mkuu wa Sudan ulioanza siku ya Jumatatu
ulitarajiwa kumalizika hapo jana lakini umeendelea hadi leo baada ya
kuongezwa siku moja ya ziada. Huu ni uchaguzi wa kwanza kufanyika tangu
kujitenga Sudan Kusini mwaka 2011.
Kiti cha urais kilikuwa kimewavutia wagombea 15 kabla ya Ahmad Radi na Omar Awadh kujiondoa. Hata hivyo Rais al-Bashir anatarajiwa kushinda tena kiti hicho baada ya vyama vikuu vya upinzani kususia zoezi hilo muhimu.

0 comments:
Post a Comment