KITUO CHA MABASI
Waziri Mkuu MIZENGO PINDA ameridhishwa na utekelezaji wa miradi ya
Miundombinu ikiwemo ya barabara na maji inayotekelezwa katika miji saba
nchini kwamba imefuata na kuheshimu thamani ya fedha iliyotolewa
kwaajili ya miradi hiyo.Waziri Mkuu PINDA ametoa kauli hiyo wakati akizindua Kituo Kikuu cha Mabasi kilichojengwa na Halmashauri ya Jiji la Mbeya kwa mkopo wa fedha zaidi ya shilingi Bilioni 2 kutoka Benki ya dunia,na kwamba Benki ya dunia itaendelea kuisaidia Tanzania kutokana na utekelezaji unaoridhisha.
Kituo cha mabasii kilichojengwa na halmashauri ya jiji la Mbeya eneo la
Nane mjini Mbeya ambacho kimekamilika kwa gharama ya zaidi ay shilingi
Bilioni 2.
KITUO KIKUU CHA MABASI WAKATI WA UJENZI WAKE
Kituo hiki cha mabasi kinazinduliwa ikiwa ni miongoni mwa miradi ambayo Benki ya Dunia imetoa mabilioni ya fedha katika miji saba na majiji Manne nchini,waziri mkuu wa jamhuri ya Muungani wa Tanzania MIZENGO PINDA motto wa mkulima ndiye aliyekizindua kituo hiki.
Kituo hiki mbali na kuwa msaada wa kushusha na kupakia abiria lakini pia kimeongeza na kupanua wigo wa ajira mkoani Mbeya.

0 comments:
Post a Comment