Thursday, 28 August 2014

 Anaitwa Patrick Ole Sosopi. Ni mmasai aliyezaliwa na kukulia mkoa Iringa, jimbo la Ismani. Ana umri wa miaka 28. Ni msomi wa shahada ya kwanza ya Biashara na utawala (rasilimali watu) kutoka chuo kikuu cha Ruaha (RUCO). Kwa sasa kazi zake ni kufuga ng’ombe. Ni Baba wa mke mmoja na mtoto mmoja. Ni mgombea wa nafasi ya umakamu mwenyekiti wa BAVICHA Bara- Taifa. Historia yake ya uongozi na uadilifu wake umekuwa hauna shaka katika vipindi mbalimbali vya maisha yake. Historia yake ya uongozi ilianzia akiwa shule ya msingi, sekondari hadi chuo kikuu cha RUCO ambapo alikuwa waziri wa Fedha kwenye serikali ya wanafunzi 2011/2012. Alijiunga rasmi na CHADEMA mwaka 2009 alipokuwa mwanafunzi wa mwaka wa kwanza akiamini ni chama pekee ambacho kina tija ya kuboresha maisha ya jamii yake ya kimasai na changamoto mbalimbali ambazo zilikuwa zikiwakabili. Ole Sosopi ni mojawapo wa waanzilishi wa CHASO mkoani Iringa, harakati zake katika jimbo la Ismani na mkoa wa Iringa kwa ujumla kila mtu anazijua.
Ameshiriki katika mchakato wa ujenzi wa chama kwenye wilaya zote za mkoa wa Iringa pamoja na Mbeya. Wakati Daudi Mwangosi akiuliwa kikatili na jeshi la Polisi alikuwa umbali tu wa mita kumi akishuhudia. Aliaminiwa na vijana wa Ismani na kupata kura zote bila kupingwa na kuwa Mwenyekiti wa BAVICHA jimbo la Ismani. Baada ya kushauriwa na kushauriana na familia yake na vijana mbambali kutoka sehemu mbalimbali za Tanzania, ameona agombee nafasi ya Umakamu Mwenyekiti wa BAVICHA Bara. Ingawa ni mojawapo wa wasomi wachache kwenye jamii ya yao, ni mtu ambaye usomi wake haujamfanya asahau mila na tamaduni za kimasai. Chakula chake, mavazi yake, desturi yake ya maisha ya kila siku ni desturi za kwao na zenye kuhuwisha Utanzania.

Related Posts:


0 comments:

Post a Comment

Translate

facebook

TANGAZA HAPA

KWA HABARI MAKINI

Napokea maoni muhimu kwa pale unapoona apakustahili kuwepo kwenye blogg yetu makini yenye lengo la kukuunganisha pamoja na kuelimishana kwa yale mazuri yote piga simu kwa chochote muhimu namba zipo apo juu