Tuesday, 17 June 2014



Serikali ya Kenya imethibitisha kutokea shambulio lingine huko Mpeketoni usiku wa kuamkia leo na kuua watu 15, wakiwemo polisi wawili katika eneo la Poromoko.
Waziri wa Mambo ya Ndani Joseph Ole Lenku amesema Washambuliaji hao waliuharibu kwanza mnara wa simu wa
kampuni ya Safaricom na baadae kuendesha mauaji hayo mapya, baada ya jana pia kuua watu 48.

Waziri Ole Lenku amesema washambuliaji hao waliharibu mawasiliano na kukwamisha mawasiliano yote ili kudhibiti wananchi wasitoe taarifa kwa vyombo vya usalama wakati wa shambulio hilo.
 
Serikali inasema kuwa wanamgambo wa Alshabaab walikata mawasiliano ya simu katika eneo hilo kabla ya kutekeleza shambulizi hilo.
Wanamgambo hao wanaohusishwa na kundi la Alqaeda wanasema kuwa wataendelea kufanya mashambulizi nchini Kenya ikiwa serikali haitaondoa wanajeshi wake nchini Somalia.
Shambulizi hilo la vijijini ni limeonekana kuwa mfumo mpya wa mashambulizi ambayo yamekuwa yakifanya na Al Shabaab ambalo mara nyingi limekuwa likilenga maeneo ya mijini hasa miji mikubwa.
Takriban watu 48 waliuawa katika mashambulizi yaliyofanyika usiku wa kuamkia Jumatatu huku washambuliaji wakishambulia hoteli na kituo cha polisi pamoja na kuteketeza magari.
 

0 comments:

Post a Comment

Translate

facebook

TANGAZA HAPA

KWA HABARI MAKINI

Napokea maoni muhimu kwa pale unapoona apakustahili kuwepo kwenye blogg yetu makini yenye lengo la kukuunganisha pamoja na kuelimishana kwa yale mazuri yote piga simu kwa chochote muhimu namba zipo apo juu

NEWS