Friday, 13 June 2014


Naipenda kazi ya kuwa mwakilishi na msemaji wa watu. Ni kazi ngumu hasa unapowakilisha eneo ambalo kwa miaka mingi hali ya maendeleo imekuwa nyuma. Watu wanaweka matumaini makubwa kwako hata kama mfumo uliopo haukupi uwezo na rasilimali za kuyamaliza matatizo yao (kama Serikali haijapanga bajeti ya kutengeneza barabara inayohitaji bilioni 12 hata uwe nia njema kiasi gani barabara itabaki mbovu). Unachoweza kufanya ni kuendelea kujaribu na kuweka ubunifu. Lakini pia kuendelea kuwa karibu nao. Heshima wanayokupa ni deni ambalo lazima ulilipe kwa kuwatumikia kwa bidii na maarifa yote. Kidogo kidogo tutafika kule tunakotarajia.

0 comments:

Post a Comment

Translate

facebook

TANGAZA HAPA

KWA HABARI MAKINI

Napokea maoni muhimu kwa pale unapoona apakustahili kuwepo kwenye blogg yetu makini yenye lengo la kukuunganisha pamoja na kuelimishana kwa yale mazuri yote piga simu kwa chochote muhimu namba zipo apo juu

NEWS