Wednesday, 21 May 2014

manzari mzuri 
Mkoa wa Iringa uko katika Nyanda za Juu za Kusini mwa Tanzania.

 Mkoa huu unapakana na ukanda mkavu wa kati wa Tanzania katika upande wa kaskazini na kupakana kusini na Ziwa Nyasa. Mkoa wa Iringa umetanda kati ya latitudo 7º 05˝ na 12º 32˝ kusini, na longitude 33º 47˝ hadi 36º 32˝ mashariki mwa Meridian. 

Mkoa wa Iringa unapakana na Mikoa ya Dodoma na Singida upande wa kaskazini, Mkoa wa Mbeya upande wa Magharibi, Mkoa wa Morogoro upande wa Mashariki na Mkoa wa Ruvuma kwa upande wa kusini. Ziwa Nyasa linatenganisha Mkoa wa Iringa na nchi ya Malawi upande wa kusini Magharibi mwa Tanzania.


Mkoa wa Iringa una eneo lenye ukubwa wa jumla ya km2 58,936.  Wastani wa asilimia 74 ya eneo hili linafaa kwa shughuli za kilimo ambalo ni sawa na km2 43,935.  Eneo linalobakia la km2 15,001 ni eneo la maji, hifadhi ya mbuga za wanyama, milima na misitu.

Related Posts:


0 comments:

Post a Comment

Translate

facebook

TANGAZA HAPA

KWA HABARI MAKINI

Napokea maoni muhimu kwa pale unapoona apakustahili kuwepo kwenye blogg yetu makini yenye lengo la kukuunganisha pamoja na kuelimishana kwa yale mazuri yote piga simu kwa chochote muhimu namba zipo apo juu